Publication
Hotuba ya Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Profesa Jumanne Abdallah Maghembe (Mb.) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa Mwaka 2011/2012
Abstract
1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo Maji na Mifugo inayohusu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, sasa lijadili na kukubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa mwaka wa Fedha wa 2011/2012.

