Back to news

News

Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 2009/10 - Mh. Lawrence Masha (MB.)

Hoja 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu, baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa mapema leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, likubali kupokea, kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya...

Hoja 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu, baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa mapema leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, likubali kupokea, kujadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha wa 2009/2010. Rambirambi 2. Mheshimiwa Spika, naomba kuungana na Wabunge wenzangu katika kutoa rambirambi zangu kwa familia na wananchi wa majimbo matatu ambayo yaliwapoteza Wabunge wao katika mwaka wa fedha wa 2008/2009. Majimbo hayo ni ya Tarime, Mbeya Vijijini na Busanda kwa kuwapoteza waliokuwa Wabunge wenzetu Waheshimiwa marehemu Chacha Wangwe, Richard Said Nyaulawa na Kabuzi Faustine Rwilomba. Namwomba Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi. Amina.